Shukrani

Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa wote waliohusika katika mchakato wa kuanzisha na kuchapisha Jarida la Dira ya Lugha (JADILU). Kwanza kabisa, tunaishukuru Idara ya Isimu, Lugha na Fasihi, Shule ya Insia na Sayansi za Jamii, Kamati ya Wativa, Kikao cha Seneti, Kamati ya Baraza la Chuo la Elimu, Utawala wa Chuo Kikuu cha SEKU na hatimaye Baraza la Chuo Kikuu cha South Eastern Kenya (SEKU) kwa kuidhinisha pendekezo la kuanzishwa kwa jarida hili. Bila michango yenu na idhini, jarida hili lisingekuwapo.

Aidha, tunatoa shukrani za pekee kwa bodi ya uhariri kwa kujitolea kusoma, kutathmini, na kutoa maoni ya kina kuhusu makala zilizopokelewa. Uchangiaji wenu umewezesha kuhakikisha kwamba jarida hili lina ubora wa juu na mchango muhimu kwa taaluma za Kiswahili.

Pia, shukrani za dhati ziende kwa Bodi ya Ushauri kwa uongozi wao makini na maelekezo yaliyoleta mafanikio katika mchakato mzima.

Tunawashukuru waandishi wote waliochangia makala zao katika jarida hili. Michango yao imewezesha kuleta maarifa mwafaka yaliyomo katika Jarida la Dira ya Lugha.

Tunapenda kutoa shukrani kwa Utawala wa Chuo Kikuu cha SEKU kwa ufadhili na uongozi mwema ambao umewezesha kutimiza azma ya kuchapisha jarida hili.

Mwisho, tunatoa shukurani za dhati kwa makatibu mhutasi (Philomena Mwende Makau, Gladys Mawia Muthengi, Jacob Mwaniki na Maina T. Sammy) walioshughulikia upokeaji na upangaji wa rasimu ya kwanza ya jarida hili.