About the Journal

MAELEZO KWA WAANDISHI WA MAKALA

Jarida la Dira ya Lugha (JADILU) lilianzishwa mwaka 2023. Hili ni jarida la kimataifa linalochapisha makala zake mara mbili kwa mwaka. JADILU ni jarida linalolenga kuchochea mijadala inayohusu Taaluma za Kiswahili zikiwemo isimu, lugha, fasihi pamoja na taaluma zinazohusiana nazo kama vile tafsiri na ukalimani. Jarida hili ni njia muhimu ya kusambaza maarifa yanayoibuliwa na tafiti mbalimbali za taaluma za Kiswahili. Jarida linapatikana katika nakala ngumu pamoja na nakala tepe ya mkondoni.

Lengo kuu la JADILU ni kukuza, kueneza na kutandawaza lugha ya Kiswahili na utamaduni wa Mswahili na Mwafrika. Hivyo, tunahimiza wanazuoni, watafiti na wataalamu mbalimbali kutuma makala za taaluma zote za Kiswahili, Tafsiri, Ukalimani na Utamaduni wa Kiswahili kutoka kote duniani kuchapishwa katika jarida la Dira ya Lugha. Tunapokea miswada iliyoandikwa kwa Kiswahili na Kiingereza na inayohusu taaluma za Kiswahili na Kiafrika.

Waandishi wa makala wanapaswa kuzingatia yafuatayo:

  1. Makala ipigwe chapa kwenye karatasi ya A4, kwa kutumia programu ya Word kwenye hati ya Times New Roman yenye ukubwa wa 12 na nafasi ya 1.5 kati ya mstari na mstari.
  2. Ukurasa wa juu wa makala uwe na: anwani (mada), jina la mwandishi/waandishi, baruapepe na jina la asasi anayojinasibisha nayo.
  3. Makala iwe imeambatana na ikisiri fupi yenye urefu wa maneno 150-250.
  4. Makala iwe na urefu kati ya maneno 3000-7500 ikiwa ni pamoja na ikisiri na marejeleo.
  5. Tanbihi zote ziwekewe namba na zitumike pale tu inapobidi.
  6. Marejeleo yafuate mfumo wa APA, Toleo la Saba.
  7. Kabla mwandishi hajatuma makala yake, aipitie kwanza vizuri na kujiridhisha kuwa makosa yote yamerekebishwa kwa kiwango kinachoridhisha.

Makala yoyote inayowasilishwa katika Jarida la Dira ya Kiswahili itapitia mchakato wa tathmini ya kina itakayofanywa na wapitimakala. Kila makala itatathminiwa na angalau wapitimakala wawili wa kitaaluma, ambao watachambua na kutoa maoni yao kuhusu ubora wa utafiti, usahihi wa hoja zilizotolewa, na mchango wa makala katika taaluma husika. Baada ya tathmini hii, makala itarejeshwa kwa mwandishi ili aweze kufanya marekebisho yoyote yanayohitajika kabla ya kuchapishwa.

Tanbihi:
Endapo kutatokea sababu zisizoepukika za juzuu lolote la JADILU kutokuchapishwa, juhudi zitafanywa kuhakikisha kuna toleo maalumu la makala zote zilizokusudiwa kuchapishwa.

Kwa mawasiliano zaidi unaweza kutumia anwani ifuatayo:
Jarida la Dira ya Lugha,
Idara ya Isimu, Lugha na Fasihi,
Chuo Kikuu cha South Eastern Kenya,
S.L.P 170-90200 KITUI-KENYA
Baruapepe: jadilu@seku.ac.ke
Simu: +254 748 605 997